“Siti Msharifu”. Neno hili tunalipata mara moja tu! Katika biblia nzima katika kitabu cha Wimbo ulio bora 7:1. Wimbo ulio bora linasoma. 7:1 “SITI MSHARIFU, jinsi zilivyo nzuri Hatua zako katika MITALAWANDA. Mapaja yako ya mviringo ni kama johari, Kazi ya mikono ya fundi mstadi” Maana ya neno hilo ni “binti wa Mfalme”.. Kiswahili cha zamani cha binti wa Mfalme ni “siti-msharifu”.. Kwahiyo katika mstari huo unaweza kusomeka kama “Binti wa mfalme, jinsi zilivyo nzuri hatua zako katika Mitalawanda”. Na neno “Mitalawanda” linapatikana mara moja tu katika biblia yote, na tunalisoma katika kitabu hicho hicho cha Wimbo ulio bora 7:1.. Na maana ya neno hilo ni “Viatu vilivyotengenezwa kwa kamba”…kwa kiingereza sandals au sendoz. Maeneo ya mashariki ya kati, watu hawakuwa wanavaa viatu kama hivi vyetu, bali vile vilivyotengenezwa kwa kamba, Kwahiyo Kiswahili cha zamani cha sendoz, ndio hiyo Mitalawanda. Hivyo Mstari huo wa wimbo uliobora 7:1, unaweza kusomeka hivi.. “Binti wa mfalme, jinsi zilivyo nzuri hatua zako katika sendozi”. Kwaujumla kitabu cha Wimbo ulio bora, kinahusu mazungumzo ya kimahusiano kati ya mtu na mke wake katika hatua tofauti tofauti, kikifunua uhusiano wetu sisi na Kristo katika hatua tofauti tofauti (yaani wakati tunampokea Yesu na baada ya kumpokea Yesu), kwasababu kimaandiko, Kristo ndiye Bwana na sisi ni bibi-arusi wake. Na neno la mwisho ni “Kulalama”. Neno hili limeonekana sehemu kadhaa katika biblia, na maana ya Neno hili ni “kuugua rohoni au moyoni, hususani kwa kuomba”.. Mtu anayeomba kwa kuugua sana, mtu huyo ni ANALALAMA! Na ni wajibu wa kila Mkristo kuomba kwa kulalama kila wakati, kwasababu kama jambo una mzigo nalo huwezi kuliombea juu juu tu!, bali utaomba kwa kuugua sana. Na jambo linaloombewa kwa mzigo mzito ni rahisi kuleta matokeo haraka sana zaidi ya lile linaloombewa juu juu tu! #trending #sda #sdachurch #wedding