Jaribio la ugaidi Mombasa

Jaribio la ugaidi Mombasa

ktnkenya.tv Polisi wa kupambana na ugaidi mjini Mombasa wanachunguza jaribio la ulipuaji katika kituo kimoja cha petroli mjini humo. Kwa mujibu wa mkuu wa upelelezi mjini humo Ambrose Munyasia, chupa iliyojazwa kemikali zinazoweza kulipuka ilirushwa katika kituo hicho na kugonga gari lililoegeshwa humo. Walioshuhudia wanasema miale ya spaki ilionekana wakati chupa hiyo iligonga gari kisha baadaye gurudumu lake likapasuka.