Rais Ruto asema hakuna mipango yoyote ya kuvuruga au kuingilia shughuli za vyombo vya habari

Rais Ruto asema hakuna mipango yoyote ya kuvuruga au kuingilia shughuli za vyombo vya habari

Rais William Ruto amesema hakuna mipango yoyote ya kuvuruga au kuingilia shughuli za vyombo vya habari. Rais akisitiza kuwa wanahabari wana uhuru wa kuendelea na kazi yao bila kuwa na hofu ya shughuli zao kuingiliwa na serikali. Alisema haya kufuatia malalamishi kutoka kwa vyombo vya habari kuwa serikali ilikuwa na mipango ya kuhitilafiana na shughuli zao.