Watu 2 waliotoroka Karantini KMTC wakamatwa wakiwa walevi chakari

Watu 2 waliotoroka Karantini KMTC wakamatwa wakiwa walevi chakari

Watu wawili kati ya hamsini waliotoroka karantini hapa Nairobi wamekamatwa huku polisi wakiwa mbioni kuwatafuta wengine waliosalia. Wawili hao walikamatwa katika mtaa wa Marurui kaunti ya Kiambu, siku ambayo serikali imetangaza kuwa idadi ya walioambukizwa imefikia 303. Na kama anavyotuarifu Chemutai Goin, Rais Uhuru Kenyatta ametoa onyo kwa wanaokamatwa wakikaidi sheria kuwa wataishia karantini.