Kinara wa ODM Raila Odinga ameahidi kuboresha sekta ya utalii maeneo ya pwani, leo hii akiendeleza ziara yake ya Pwani kaunti ya Kilifi. Raila akisema kuwa ataanza kuangazia manifesto yake rasmi atakapotangaza azma yake ya urais mwezi ujao huku akitarajiwa kaunti ya Kwale hapo kesho.