Waziri wa Usalama Joseph Ole Lenku amesema kuwa serikali iko kwenye harakati ya kuweka maafisa wa usalama kwenye maeneo mbalimbali, katika mradi wa jamii kushirikiana na maafisa wa usalama ili kuangamiza visa vya uhalifu. Ole Lenku aliyasema haya katika mkutano na makamishna wa kaunti walipokuwa wakijadili maswala ya usalama.