Timu ya taifa ya Tanzania, #TaifaStars imefanya come-back na kuichapa Senegal 2-1 katika mchezo wa mwisho wa kuhitimisha michuano ya CECAFA 3 Nations Tournament, kwenye Uwanja wa Black Rhino, Karatu Arusha... Senegal wametangulia kuapata bao kipindi cha kwkanza kupitia kwa Mapathe Mbodji, lakini Tanzania ikachomoa kwa penati ya Abdul Suleiman Sopu dakika ya 53 kabla ya Ibrahim Hamad Abdullah 'Bacca' kufunga la pili dakika ya 57.... Kwa matokeo haya, Tanzania ndiyo bingwa wa michuano hiyo ikiwa imemaliza na pointi sita, ikifuatiwa na Uganda wenye alama tatu huku Senegal wakiondoka bila alama yoyote baada ya kupoteza mechi za o zote mbili... Mashindano haya yalishirikisha timu za Tanzania, Uganda na Senegal, ikiwa ni maandalizi ya fainali za CHAN2024